Mahojiano: Prof. Sakamoto Kumiko wa Chuo Kikuu cha Utsunomiya
Hiki ni kipindi ambacho tunasoma barua yako msikilizaji kuhusu maoni ya vipindi mbalimbali ambavyo tunavitangaza kwenye Idhaa yetu ya Kiswahili. Pia tutakuwa na mahojiano na Prof. Sakamoto Kumiko wa Chuo Kikuu cha Utsunomiya, UU ambaye amekuwa akiendesha mradi unaohusisha vyuo vikuu 7 kutoka Japani na Afrika ili kuendeleza rasilimali watu. Mwezi Machi, aliandaa mkutano uliojulikana kama "UU-A Student Summit 2022" uliohudhuriwa na wanafunzi 53 kutoka Japani na Afrika waliowasilisha mada mbalimbali. Aidha kuanzia leo, tunatambulisha "Kifahamu Kijapani," kona itakayokuwezesha kuifahamu lugha ya Kijapani kupitia habari.
Prof. Sakamoto Kumiko wa Chuo Kikuu cha Utsunomiya.
Sloane Mungai ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, JKUAT nchini Kenya. Alifanya wasilisho lililochaguliwa kama moja kati ya 10 bora.
Lilian Kakoko ni mwanafunzi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, NM-AIST. Anadhamiria kushiriki mkutano utakaofanyika mwaka 2023.