Mgeni wetu wa leo ni dada Masayo.
Hiki ni kipindi ambacho tunasoma barua yako msikilizaji kuhusu maoni ya vipindi mbalimbali ambavyo tunavitangaza kwenye Idhaa yetu ya Kiswahili.

Mgeni atakayetupambia kipindi chetu wiki hii ni dada Masayo, Mjapani msanii na mwimbaji aliyewahi kuishi nchini Tanzania kwa muda wa miaka 8. Nini mtazamo wake kuihusu Tanzania, na alivutiwa na nini nchini humo? Yote hayo utayabaini katika kipindi Ukumbi wa Jumapili.