Pambo la Mlima Fuji katika "cloisonné" lililotengenezwa na Sousuke Namikawa
Tutaangazia picha ya "cloisonné" ya Mlima Fuji. "Cloisonné" hiyo imetengenezwa kwa kuweka enameli- aina ya gilasi- kwenye kitako cha chuma kwa kutumia joto. Kazi hiyo ilifanywa na Sousuke Namikawa, mmoja wa mafundi stadi maarufu wa "cloisonné", kwa ajili ya kuonyeshwa katika Maonyesho ya Biashara ya mwaka 1893. Picha ya Mlima Fuji uliyotokeza kwenye mawingu kana kwamba umechorwa pia ulibeba matarajio motomoto ya Japani ya nyakati hizo.