Somo la 43: Unaonekana mwenye afya.
Tam amekwenda kwenye onyesho la piano la mwanamume anayempenda, Yuuki, pamoja na Mi Ya. Baada ya onyesho wawili hao wanakwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Yuuki ili kumsalimia. Tam amemletea Yuuki shada la maua. Katika somo hili utajifunza namna ya kuelezea fikra kuhusu unachokiona. Baadaye kwenye kipindi tutazungumzia maua nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika.
Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.