Somo la 42: Ninadhamiria kumpatia Yuuki-san.
Tam amefahamu kwamba Yuuki, mpiga piano anayempenda, atafanya onyesho. Hivyo yeye na rafikiye Mi Ya wapo kwenye ukumbi wa tamasha siku ya onyesho. Katika somo hili utajifunza namna ya kuelezea dhamira au mipango yako. Baadaye kwenye kipindi tutazungumzia makasri ya Kijapani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.