Somo la 41: Tunaweza kununua tiketi?
Mi Ya anaperuzi mtandaoni chumbani kwake na kuona kitu kilichomshangaza. Anamwita Tam. Katika somo hili utajifunza namna ya kuuliza iwapo jambo unalolitaka linawezekana. Baadaye kwenye kipindi tutakujuza juu ya Kabuki, moja ya tamaduni za maonyesho ya jukwaani ya Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.