Somo la 40: Kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza, nimeshtuka.
Tam na Mi Ya wametulia zao sebuleni kwenye "Nyumba ya Haru-san." Ghafla sensa za Haru-san, mwenyenyumba roboti zikabaini kitu kisicho cha kawaida. Katika somo hili utajifunza namna ya kuelezea sababu. Baadaye kwenye kipindi tutazungumzia cha kufanya pindi linapotokea tetemeko la ardhi.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.