Somo la 39: Nimepoteza pochi yangu.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu anaharaka kurejea nyumbani. Amepoteza pochi yake akiwa njiani kutoka kituo cha treni. Anamwomba ushauri Haru-san, mwenyenyumba roboti. Katika somo hili utajifunza namna ya kuelezea kosa ulilofanya. Baadaye katika kipindi tutazungumzia vituo vya polisi vya Japani viitwavyo "koban."

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.