Somo la 38: Nje ni bora.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu yupo safarini Hakone na rafiki yake Ayaka. Wamo kwenye meli ya kitalii kwenye Ziwa Ashinoko. Kwenye somo hili utajifunza namna ya kulinganisha vitu viwili tofauti. Baadaye tutazungumzia mlima Fuji.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.