Somo la 37: Runinga haiwaki…
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu amezuru Hakone na rafikiye Ayaka. Wamejisajili kwenye hoteli ya chemchemi ya majimoto, lakini inaonekana kuna tatizo chumbani mwao. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kusema kuna tatizo. Baadaye tutazungumzia hoteli za Kijapani, ziitwazo "ryokan."

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.