Somo la 35: Ninataka kwenda Owakudani na kula mayai meusi.
"Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu na rafikiye, Ayaka wanaelekea Hakone, eneo maarufu la kitalii lililpo jirani na Tokyo. Ndani ya treni wanajadili cha kufanya watakapofika huko. Katika somo hili utajifunza kuelezea vitendo vya wakati uliopita au ujao kwa mtiririko, na baadaye utafahamu kuhusu Hakone, eneo la kitalii la jirani na Tokyo.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika.
Bofya tu linki iliyo chini ya picha."
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.