Somo la 34: Nimewahi kukisoma.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu na Mike wamefika kwenye "manga café," ambapo kuna mkusanyiko wa vitabu vingi vya katuni za manga pamoja na majarida na unaweza kuvisoma utakavyo. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kusema ulichowahi kukifanya na kisha utafahamu kuhusu "manga café."

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.