Somo la 33: Nitasubiri kwa muda gani?
Kaito na Mike wamefika salama kwenye Makumbusho ya Ninja mkoani Mie. Wameamua kujaribu kutumia silaha za ninja za shuriken. Kuna foleni ndefu eneo hilo. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuuliza kitu fulani kitachukua muda gani na kisha utafahamu juu ya utalii wa kujaribu kufanya vitu nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.