Somo la 30: Tuliimba nyimbo na kucheza dansi pamoja.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu amefika mgahawani na Mi Ya, mpigapicha kutoka China. Tam anazungumzia kumbukumbu zake kuhusu mwanafunzi wa muziki, Yuuki. Kwenye somo hili utajifunza jinsi ya kuelezea mambo mbalimbali uliyoyafanya na utakayoyafanya. Na kisha utafahamu kuhusu vitamutamu vya Kijapani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.