Somo la 29: Nilikwenda kusikiliza onyesho la piano.
Kwenye nyumba ya Haru-san, Mi Ya anazungumza na Tam na mwenyenyumba wao huku akiwaonesha picha alizopiga kwenye onyesho la kupiga piano Kamakura. Tam anazitazama na kushangazwa mno. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kusema ulichokifanya na baadaye utafahamu kuhusu Kamakura, eneo maarufu la kitalii.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.