Somo la 28: Ninaweza kupiga picha?
Mi Ya amefika hekalu la Kamakura ili kupiga picha. Tamasha la piano kwa ajili ya kuchangisha fedha linafanyika huko. Kwenye somo hili utajifunza jinsi ya kuomba ruhusa. Na baadaye utafahamu kuhusu muziki Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.