Somo la 27: Kipi ni kitamu zaidi?
Kaito amempeleka Tam kwenye mgahawa wa tambi za rameni jijini Tokyo. Huko, Tam anamkumbuka Yuuki, mwanafunzi wa muziki anayempenda na aliyekutana naye katika kazi ya kujitolea nchini Vietnamu. Kwenye somo hili utajifunza jinsi ya kuuliza kipi cha kuchagua na baadaye utafahamu kuhusu tambi za nudo na rameni, chakula maarufu duniani kwa sasa.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.