Somo la 26: Hiki kimanda cha Kijapani ni kitamu na kina ladha nzuri.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnam, Mi Ya, Kaito na mwenye nyumba wao Haru-san wamefika kwenye bustani kwa ajili ya ohanami. Ohanami ni utamaduni wa Kijapani wa kutazama maua ya mcheri huku ukizunguka zunguka na kupumzika chini ya miti. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuelezea fikra mbalimbali. Na baadaye utafahamu kuhusu Ohanami.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.