Somo la 25: Koo langu linauma.
Tam ametulia sebuleni, lakini hajihisi vizuri leo. Katika somo hili utajifunza namna ya kusema hujihisi vizuri na baadaye utafahamu kitu gani ufanye pindi utakapoumwa nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.