Somo la 23: Mimi nampenda paka huyu.
Tam, amerejea jijini Tokyo baada ya safari yake ya Hokkaido. Hivyo yeye, Ayaka na Mike Mmarekani anayefahamu mengi kuhusu utamaduni wa Japani, wamefika kwenye mgahawa wa kipekee unakoweza kutangamana na paka, huku ukifurahia kahawa au chai yako. Katika somo hili utajifunza kuelezea unachokipenda na kisha baadaye utafahamu kuhusu aina tofauti za migahawa ya kipekee inayopata umaarufu nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.