Somo la 22: Tupige picha.
Tam, Mi Ya na Kaito wapo jijini Sapporo mkoani Hokkaido. Wamefika kwenye tamasha la theluji, na wapo mbele ya sanamu kubwa ya kasri lililotengenezwa kwa theluji. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kumwambia mtu ufanye naye kitu pamoja. Na baadaye, utafahamu kuhusu Hokkaido, eneo maarufu la kitalii.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.