Somo la 21: Nipo ndani ya mnara wa saa.
Tam na Mi Ya wapo Hokkaido. Leo, wanatakiwa kukutana na Kaito kwenye eneo maarufu la kitalii, Mnara wa Saa wa Sapporo. Tam anapokea simu kutoka kwa Kaito wakati yeye na Mi Ya wakisubiri ndani ya mnara. Kwenye somo hili utajifunza jinsi ya kusema mahali au sehemu ulipo, na kisha tutaangazia kuhusu maduka ya saa 24 nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika.
Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.