Somo la 20: Tafadhali usiweke kiungo cha wasabi.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu, na Mi Ya wamefika Hokkaido. Wanaingia mgahawani karibu na soko la samaki jijini Sapporo ili kufurahia chakula cha baharini. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kumwomba mtu asiweke kitu fulani kwenye chakula au kinywaji chako. Na baadaye utafahamu kuhusu chakula cha baharini cha Hokkaido.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.