Somo la 19: Nahitaji jozi ya glavu.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu, anapanga kwenda Hokkaido kaskazini mwa Japani. Ili kujiandaa kwa baridi kali ya Hokkaido, yeye na Mi Ya, wanakwenda kununua glavu. Katika somo hili utajifunza namna ya kusema unachotaka kununua, na baadaye utafahamu kuhusu matumizi ya kadi za mkopo nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.