Somo la 18: Kulifurahisha kweli.
Mi Ya, mpigapicha kutoka China, amerejea kutoka Nagano alikokwenda kupiga picha. Yupo sebuleni kwenye "Nyumba ya Haru-san," akiwaelezea Tam na mwenyenyumba roboti Haru-san kuhusu safari yake. Katika somo hili utajifunza namna ya kuelezea mvuto wa ulichokifanya. Na baadaye utafahamu kuhusu treni za mwendokasi za Shinkansen.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.