Somo la 17: Nimekuwa nikisafiri sehemu mbalimbali Japani.
Mi Ya anapiga picha kwenye chemchemi ya majimoto mkoani Nagano, ambappo nyani huoga humo. Amekutana na wanandoa Wajapani ambao wanatalii pia, na wanaenda kwenye mgahawa wa tambi za soba. Katika somo hili utajifunza namna ya kuwaambia watu kile ambacho umekuwa ukikifanya au unachokifanya kwa sasa. Na kisha utafahamu kuhusu chakula cha kitamaduni cha Kijapani, tambi za soba.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.