Somo la 16: Hii ni chemchemi maarufu ya majimoto.
Mpigapicha kutoka China, Mi Ya, yupo katika chemchemi ya majimoto ya mkoani Nagano ambayo ni maarufu kwa nyani wa porini kuoga hapo. Wakati akipiga picha wanandoa Wajapani wanaanzisha mazungumzo naye. Katika somo hili utajifunza namna ya kuelezea kuvutiwa kwako na kuelezea vitu, baada ya kujifunza katika somo la 12.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.