Somo la 15: Naelekea chemchemi ya majimoto ya nyani, tafadhali.
Mi Ya, mpigapicha kutoka China, amefika kwenye mkoa wa Nagano uliopo Japani ili kupiga picha katika chemchemi ya majimoto. Amejaribu kupanda teksi kuelekea kwenye bustani inayoitwa Jigokudani Yaen Koen. Ni eneo maarufu la kitalii ambapo nyani huoga kwenye chemchemi ya majimoto wakati wa msimu wa baridi. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kumwambia dereva wa teksi mahali unakokwenda. Na kisha utafahamu kuhusu teksi za nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.