Somo la 14: Ningependa kwenda Japani.
Katika mazungumzo ya leo utasikia kumbukumbu za Tam. Kabla ya kuja Japani, Tam alikuwa mfanyakazi wa kujitolea katika shule ya msingi nchini Vietnamu. Siku moja, Yuuki, mwanafunzi wa shule ya muziki kutoka Japani alifika kuwapigia piano watoto wa shule hiyo. Tam alivutiwa na onyesho lake na akapata ujasiri wa kuzungumza naye kwa Kijapani. Katika somo hili utafahamu namna ya kuelezea matamanio yako na baadaye utabaini kuhusu miereka ya sumo.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika.
Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.