Somo la 13: Nataka kutazama theluji.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu anazungumza na mwenyenyumba roboti, Haru-san, pamoja na Mi Ya, mpigapicha, katika sebule ya "Nyumba ya Haru-san." Katika somo hili utajifunza namna ya kuwaambia watu unachotaka kufanya. Na baadaye utafahamu kuhusu nyumba za Kijapani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.