Somo la 11: Kuna hirizi za bahati?
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu na Mi Ya, mpigapicha kutoka China wamefika eneo maarufu la kitalii la Asakusa. Wawili hao wanazunguka zunguka katika maduka ya zawadi kwenye barabara ya "Nakamise" ya kuelekea hekalu la Sensoji. Katika somo hili utajifunza semi za kuuliza iwapo kitu unachokitaka kipo. Na baadaye utafahamu kuhusu eneo la kitalii la Asakusa lililopo Tokyo.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika.
Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.