Somo la 9: Hii ni nini?
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu amefika kwenye duka la vyakula vilivyo tayari kuliwa lililopo chini ya ardhi kwenye jengo lenye maduka makubwa, linaloitwa "depa-chika," akiwa na Kaito mpangaji mwenzake pamoja na rafiki yake Mmarekani, Mike. Katika somo hili utajifunza semi za kuulizia vitu usivyovijua. Na baadaye tutaelekea "depa-chika."

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.