Somo la 6: Treni hii inakwenda Ikebukuro?
Ni siku ya kwanza ya Tam kwenda katika chuo kikuu chake jijini Tokyo kwa treni. Yupo kituo cha treni, lakini hana uhakika kama treni hiyo anayotaka kupanda ndiyo sahihi. Hivyo anamuuliza mhudumu wa kituoni hapo. Katika somo hili utajifunza namna ya kuulizia linakoelekea basi, treni na vyombo vingine vya usafiri wa umma. Vilevile tutakujuza kuhusu mfumo wa reli nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.