Somo la 5: Nimejifunza kwa kusikiliza redio
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu anaishi kwenye nyumba ya Haru-san. Leo ni siku ya kwanza ya masomo katika chuo kikuu atakachokuwa anasoma. Haru-san mwenyenyumba wake ambaye ni roboti anagundua kuwa Tam ana mashaka. Katika somo hili utajifunza semi za kuelezea namna ulivyojifunza Kijapani. Na kisha tutaangazia semi za unyenyekevu.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maansishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, shemsha bongo na kashalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.