Somo la 4: Nitasoma Kijapani katika chuo kikuu.
Tam mwanafunzi kutoka Vietnam na mpangaji mwenziwe, Mi Ya ambaye ni mpigapicha kutoka China, wamekuwa marafiki. Wanazungumza kwenye chumba cha Mi Ya. Leo utajifunza namna ya kusema unachotarajia kufanya nchini Japani. Na baadaye utajifunza pia kuhusu uzuri wa sehemu mbalimbali za Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maansishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, shemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.