Somo la 3: Ninatokea Vietnamu.
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu, ameshakutana na mwenyenyumba wake ambaye ni roboti, Haru-san, kwenye Nyumba ya Haru-san atakakokuwa anaishi akiwa nchini Japani. Leo ni karamu ya kumkaribisha na wapangaji wenziwe wanajitambulisha. Katika somo hili utajifunza namna ya kusema unakotokea. Baadaye utajifunza pia kuhusu namna ya kusalimia watu nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maansishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.