Somo la 2: Mimi ni Tam. Ni mwanafunzi.
Wakati Tam akitafuta nyumba atakayokuwa anaishi nchini Japani, amekutana na Kaito na Mi Ya, wapangaji wa nyumba hiyo pia. Wameongozana na Tam kuelekea nyumba hiyo. Kwa mshangao Tam anakutana na mwenyenyumba roboti, Haru-san. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kujitambulisha pamoja na herufi za Kijapani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti na maandishi zinazopakuliwa, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.