Kipindi Maalum ~Tutajibu swali lako~ sehemu ya 2
Hiki ni kipindi cha pili kati ya vipindi viwili maalum vinavyojibu maswali ya wasikilizaji wa "Jifunze Kijapani." Katika nusu ya kwanza, tunaelezea namna baadhi ya wasikilizaji wetu nchini Japani wanavyotumia kipindi chetu katika masomo yao. Katika Chuo Kikuu cha Aizu mkoani Fukushima, wanafunzi Wajapani wanawasaidia wanafunzi wa kigeni kujifunza Kijapani. Kipindi cha lugha pia kinatumika kama jukwaa muhimu la mabadilishano ya kitamaduni. Katika sehemu hii ya pili, msimamizi wetu wa kipindi, Isomura Kazuhiro kutoka Japan Foundation, anajibu maswali yanayohusu Kijapani na namna ya kujifunza lugha hiyo. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 27, 2021.)
Kashimoto Kimika na mwanafunzi wa kigeni Nidul Devapriya.
Tazaki Hiroshi na mwanafunzi wa kigeni Divij G. Singh.
Kusakari Akemi, Profesa Mshiriki, Chuo Kikuu cha Aizu.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.