Hiki ni kipindi cha kwanza kati ya vipindi viwili maalum vinavyojibu maswali ya wasikilizaji wa "Jifunze Kijapani." Katika nusu ya kwanza, tunaelezea namna baadhi ya wasikilizaji wetu nje ya nchi wanavyotumia kipindi chetu katika mafunzo yao. Baba na bintiye nchini India wanasema wanafurahia zaidi kujifunza Kijapani. Profesa anayefunza Kijapani nchini Brazil anaelezea anavyotumia "Jifunze Kijapani" katika masomo yake ya mtandaoni kuwafunza wanafunzi wa sekondari ya chini na juu. Pia tunawatambulisha wanafunzi wake wanaojitwika changamoto mpya ya kujifunza Kijapani licha ya panda shuka zilizosababishwa na janga la virusi vya korona. Katika nusu ya pili, msimamizi wa kipindi, Fujinaga Kaoru wa Japan Foundation, anajibu maswali yanayohusu nambari na herufi katika Kijapani na mengineyo. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 20, 2021.)
Pratyancha na daftari lake.
KC Pal na bintiye Pratyancha.
Fujiwara Mari, Profesa Mwalikwa, Chuo Kikuu cha Jimbo cha Rio de Janeiro.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.