Somo la 47: Unafanyaje?
Tam yupo Kyoto pamoja na wakazi wengine wa "Nyumba ya Haru-san." Wanazuru hekalu la Fushimi Inari Taisha. Ni maarufu kwa maelfu ya malango yake yenye rangi nyekundu ambayo yamejipanga kama njia ya chini ya ardhi. Tam anataka kucheza bahati nasibu ya "omikuji," ni karatasi ya kiagua bahati. Kwenye somo hili, utajifunza namna ya kuuliza jinsi ya kufanya kitu. Baadaye kwenye kipindi, tutazungumzia karatasi za viagua bahati vya Japani vinavyoitwa "omikuji."

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.