Tam anazungumza na mwenyenyumba roboti Haru-san katika sebule ya nyumba anayoishi. Inaonekana ana ombi. Katika somo hili, utajifunza namna ya kuomba kiungwana. Baadaye kwenye kipindi, tutazungumzia jinsi ya kufanya manunuzi nchini Japani.
Pia tuna tovuti iliyosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni za anime za mazungumzo ya somo, chemshabongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.