Somo la 44: Nimesikia onyesho lingine litafanyika.
Tam alikwenda kwenye onyesho la piano la Yuuki, mwanamume anayempenda na hatimaye aliweza kuonana naye tena. Baada ya kurudi nyumbani katika "Nyumba ya Haru-san," anawasimulia mwenyenyumba wake roboti na mpangaji mwenziwe Kaito onyesho lilivyokuwa. Katika somo hili utajifunza namna ya kumwambia mtu ulichokisikia. Baadaye katika kipindi tutazungumzia matamasha ya Kijapani.
Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.