Somo la 12: Hii ni hirizi nzuri, sivyo?
Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu, na Mi Ya, mpigapicha kutoka China, wapo kwenye Hekalu la Sensoji katika eneo la Asakusa. Wapo kwenye sehemu inayouza hirizi. Katika somo hili utajifunza namna ya kuelezea kuvutiwa kwako na kuelezea vitu. Baadaye utafahamu kuhusu mahekalu ya Shinto na kibuddha nchini Japani.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika.
Bofya tu linki iliyo chini ya picha.
Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.