Kumbukizi za Majanga Yaliyotokea Zamani
Vipande vya mawe na minara ya kumbukumbu iliyoandikwa habari na mafunzo ya majanga imesimikwa kote nchini Japani ili kubakisha kumbukumbu za matukio hayo. Iwate ni moja ya eneo lililoathiriwa vibaya na Tetemeko Kuu la Japani Mashariki na Tsunami mnamo mwaka 2011, ni mkoa wenye idadi kubwa ya mawe ya kumbukumbu za majanga ya asili. Mwanahabari wetu Bobby Judo anatembelea eneo hilo na kutalii katika baadhi ya minara na majengo ya makumbusho ya kimbunga akiwa na mwongozaji wa eneo hilo ili kujifunza busara za BOSAI. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 30, 2022.)
Katika jiji la Rikuzentakata mkoani Iwate, baadhi ya majengo yaliyoharibiwa na tsunami yamehifadhiwa ili kurithisha kumbukumbu za janga hilo. Yanaitwa "majengo ya kumbukumbu ya tetemeko la ardhi."
Mwongozaji wetu, Kono Masayoshi, ni manusura wa Tetemeko Kuu la Japani Mashariki na Tsunami.
Jiwe la kumbukumbu ya tsunami ya mwaka 1933. Limeandikwa mafunzo kama "Endapo ukisikia kishindo baada ya tetemeko la ardhi, tarajia tsunami."
Shule hii ya sekondari ya chini, aliyosoma Kono ilikumbwa na tsunami kubwa ambayo ilifika juu ya paa lake kwa urefu wa mita 14.2.