Inapokuwa Vigumu Kurejea Nyumbani Tetemeko la Ardhi Litokeapo Mjini
Utafanya nini tetemeko kubwa la ardhi likitokea ukiwa katika mji mkubwa? Kipindi hiki kinakupa vidokezo vya namna ya kujilinda hali ya dharura kama hiyo itokeapo. Ni kawaida kwa tetemeko kuvuruga usafiri wa umma, na kuacha halaiki ya watu wakiwa wamekwama sehemu za mijini. Tunajifunza cha kufanya tetemeko kubwa likitokea ukiwa mjini kwa kuigiza janga katika eneo la Shibuya jijini Tokyo. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 30, 2022.)
Bobby aliigiza cha kufanya ikiwa tetemeko la ardhi litatokea Shibuya akiwa na Yukihiro Katsuya wa Idara ya Kusimamia Majanga ya Mji wa Shibuya. Aligundua kuwa majengo mengi ya Shibuya yana vioo.
Jengo kubwa la kibiashara lililopo karibu na kituo cha Shibuya linageuzwa kuwa makazi ya muda kwa watu wasioweza kurejea nyumbani janga litokeapo. Limetengenezwa ili kutoshea zaidi ya watu 1,700 kwa siku tatu.
Ramani zikionyesha maeneo ya vilipo vituo vya watu kukaa ikiwa watashindwa kurejea nyumbani litokeapo janga, zimewekwa Shibuya. Ramani hizo ni muhimu mitandao ya simu inapokatika.