Japani ni nchi yenye hatari ya mara kwa mara ya matetemeko ya ardhi, ina mfumo wa kutuma tahadhari kupitia televisheni na simu za mkononi ikiwa kutatabiriwa kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi. Tunapopokea tahadhari hiyo, nini tunatakiwa kufanya? Katika kipindi hiki, tunajifunza jinsi ya kujilinda katika hali mbalimbali na mwanahabari wetu, Janni Olsson. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 2, 2022.)
Janni amesimama mbele ya "gari linaloigiza temeko la ardhi," ambalo linaweza kutoa tena mitikisiko ya matetemeko yaliyowahi kutokea nchini Japani.
Janni alijaribu tetemeko la kuigiza lililoupiga mkoa wa Kumamoto mwaka 2016 na kuweka rekodi ya kiwango cha juu zaidi ambacho ni namba7 kwenye kipimo cha tetemeko la ardhi kinachoanzia 0 hadi 7.
Tabia zinazopendekezwa za tetemeko la ardhi zinatofautiana kwa kutegemea pale ulipo wakati tetemeko linapiga. Mtaalam wa kuzuia maafa Sawa Yoshihiro anaelezea hatua za awali zinazohitajika katika kukabiliana na hali fotauti tofauti.
Kwa mfano, endapo tetemeko la ardhi linatokea wakati unatembea katika eneo la makazi, unatakiwa kuchutama katikati ya eneo. Kujikinga katika jengo lenye kuta za zege kunaweza kuwa hatari, kwani linaweza kuporomoka.