Mawingu ya Kumulasi ni marefu, ni mawingu yanayofanana na mlima na huonekana tu wakati wa majira ya joto nchini Japani. Huashiria uwezekano wa janga kubwa la hali ya hewa. Katika kipindi hiki, utajifunza kuhusu matukio hatari ya hali ya hewa yanayosababishwa na mawingu ya kumulasi, namna ya kubashiri yanapokaribia, na jinsi ya kujikinga na majanga kama hayo. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 5, 2022.)
Mawingu ya Kumulasi huleta mvua kubwa za kimaeneo.
Mwanahabari Bobby Judo anafanya mahojiano na mtabiri wa hali ya hewa Sasaki Kyoko.
Aina nne za matukio hatari ya hali ya hewa yanayosababishwa na mawingu ya Kumulasi: 1- Mvua kubwa, 2- Radi, 3- Mvua ya mawe na 4-Vimbunga.