Miigo ya Mafuriko na Dhoruba ya Mvua
Japani ni nchi inayokumbwa na mafuriko na mvua kubwa husababisha uharibifu mkubwa kila mwaka. Tutafanya nini ikiwa mafuriko makubwa yatatokea? Mwanahabari wetu, Janni Olsson anajifunza namna ya kujiandaa dhidi ya majanga au namna ya kukabiliana na majanga kama hayo kupitia miigo. (Kipindi hiki kilitangazwa Juni 1, 2022.)
Mvua kubwa zinaposababisha mafuriko, watu hukwama ndani ya majengo. Janni anabaini namna shinikizo linavyowekwa kwenye mlango wakati jengo linapokumbwa na mafuriko.
Wageni wanaweza wakajifunza juu ya hatari mbalimbali za mafuriko kwenye Kituo cha Mafunzo ya Usalama wa Maisha cha Honjo cha Idara ya Zimamoto ya Tokyo.
Tamura Hitoshi (kulia), ambaye ameona maeneo mengi ya majanga kama mzimamoto, anamtembeza Janni kituoni hapo.
Hali inakuwaje unapotembea nje wakati wa kimbunga? Janni anajaribu kusimama dhidi ya upepo wa kasi ya mita 30 kwa sekunde na mvua ya mililita 50 kwa saa kwenye chumba cha mwigo wa kimbunga.