Tajiriba ya Kupiga Kambi Nyumbani kwa Wanaohama
Endapo tutapata hifadhi katika kituo cha wanaohama baada ya kutokea kwa majanga kama vile kimbunga na mvua kubwa, ni aina gani ya maisha tunapaswa kutarajia? Katika kipindi hiki, tunaigiza maisha katika makazi ya muda kwa kuweka kambi nyumbani. Wasikilizaji watajifunza, miongoni mwa mambo mengine, namna ya kutengeneza kitanda kizuri na kuandaa chakula kwa kufuata masharti.
Hattori Shingo, mtaalam wa kambi za kuzuia maafa, anaonyesha namna ya kuigiza maisha wakati wa kuhama kwa familia ya mkurugenzi wa programu hiyo.
Hema linalohamishika limewekwa ndani ya nyumba. Hivi karibuni, serikali nyingi za maeneo zinaandaa mahema kama hayo. Yanatumika kulinda faragha katika makazi ya muda.
Vitanda vinatengenezwa katika mahema kwa kutumia kadibodi, mablanketi, magodoro ya kujaza hewa na kadhalika. Kulala vizuri ni muhimu ili kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na uhamaji.
Familia inajaribu kupika mchele kwa kutumia mifuko ya plastiki: Weka mchele katika mfuko wa plastiki unaozuia joto, mimina maji, funga mfuko na uache mchele ulowe kwa muda wa saa moja. Kisha upashe joto mfuko wako katika maji yanayochemka na utakuwa umemaliza.