Kujikinga dhidi ya Ugonjwa Unaosababishwa na Joto Kali
Ongezeko la halijoto ni hali inayoshuhudiwa duniani. Nchini Japani, joto la majira ya joto linaendelea kuwa kali zaidi kila mwaka, na kufanya ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali kuwa shaka kuu. Hali hii inasababisha kizunguzungu na viungo kufa ngazi na inaweza kusababisha kifo. Katika kipindi hiki, tutajifunza namna ya kukabiliana na ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali, na tunachopaswa kufanya ili kuuzuia.
Mwanahabari wetu, Bobby Judo, akijaribu bidhaa mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali katika 'Maonyesho ya Kukabiliana na Joto Kali.'
Jaketi lililofungwa feni za kutoa ubaridi kuzunguka kiuno linavutia nadhari ya dunia.
Kifaa hiki kinapima WBGT, kipimo kinachotumiwa kukadiria hatari ya ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali. Kinapozidi 28, hatari ya ugonjwa huo kutokea ni kubwa.
Bobby akimsikiliza Miyake Yasufumi, Mkurugenzi wa Kituo cha Matibabu Maalum cha Chuo Kikuu cha Teikyo, kuhusu namna tunavyoweza kujilinda wenyewe dhidi ya ugonjwa wa kuzirai kutokana na joto kali.